Ki msingi sio jambo la kuamka tu siku moja ukaanza kununua kwenye
mtandao, ni lazima upitie hatua kadhaa kabla ya kuanza rasmi kununua kwenye
mtandao. Jambo la kwanza, fungua akaunti katika benki yoyote yenye huduma za
kimataifa kama vile CRDB, NBC, EXIM BANK nk ambazo zina huduma za master card
na visa. Kwa NMB hadi niandikavyo maelezo haya ni kwamba hawana huduma za
mastercard na/au visa. Ukishafungua akaunti hakikisha unapewa ile kadi ya ATM
(credit/debit card), mara nyingi benki zetu Tanzania hutoa debit cards.
Sasa baada ya kuwa
umeshafungua akaunti kwenye bank yoyete kisha ukapata kadi ya atm yenye nembo
ya mastercard na / au visa, kinachofuata rudi bank uwaombe ili waiwwzeshe
akaunti yako kufanya malipo kwwnye mtandao (online purchaising). Bank watakupa
fomu maalumu utaijaza kisha ujikomiti kwa lolote litakalotokea katika shughuli
yako ya kulipa kwenye mtandao, utaweka sahihi yako kisha wakabidhi hiyo fomu na
utaambiwa kusubiri kwa muda usiopungua siku tatu (wakati mwingine unawwza
kusubiri hadi mwezi mzima kutegemea na uharaka wa benki husika).
Kuna watu wengi
waliwahi kuniuliza ni bank gani inafaa kuitumia kama debit card issuer kwenye
manunuzi mtandaoni. Jibu sio rahisi kupatikana maana sijawahi kutumia banki
zote, hata hivyo mimi ni mteja wa CRDB na ninazo sababu za kupenda kutumia
CRDB. Hebu angalia mfano Standard Chartered au Exim Bank, hutakiwi kufungua
akaunti kule kama wewe ni mtanzania mwenye kipato cha chini au kawaida. Huduma
zao ni ghali sana na hakuna huduma ya bure. Wakati huu naandika maelezo haya,
Standard Chartered wanatoza dola kumi kila mwezi kutoka kwenye akaunti yako
pamoja na asilimia zingine zaidi kila unapotumia huduma zao. Kwa CRDB hayo
malipo hayapo, hukatwi hela hizo. Mimi sio afisa wa CRDB ila ni mteja na
ninaongea na jamii yenye utambuzi na uhuru wa kuchagua huduma toka benki
yoyote.
Baada ya kuwezeshwa
kadi yako sasa unastahili pongezi maana unaweza kununua unachotaka kutoka
mtandaoni na kwa muda wowote hata kama umelala kitandani. Lakini pia sio kulipa
tu bali hata kulipwa au kupokea malipo kwa njia hiyo ya kadi yako (Jinsi ya kupokea malipo kwa paypal na
moneybookers). Lakini pia lazima ukumbuke kuwa kuna mitandao mingine sio
salama kufanya malipo kwa kadi yako, unaweza ukalipa ukajikuta pesa yote haimo
kwenye akauntu na utalia. Hivyo imekupasa kuchukua tahadhali kubwa na kuangalia
mitandao unayotumia kununua au kulipa. Na ili uwe salama na pesa yako kwa
asilimia nyingi, zipo njia na mifumo salama unayopaswa uitumie kwa usalama wa
pesa zako.
Ushauri wangu,
jiunge na ebanking, mimi ni mteja wa CRDB hivyo sijui benki zingine wanaitaje
hiyi huduma. Ukishajiunga na ebanking utaweza kupokea, kutoa au kutumia pesa
kwenye akaunti yako kwa njia ya mtandao kwa kutumia komputa au simu yako kama
imeunganishwa naaa internet. Hadi naandika maelezo haya ni kwamba CRDB wanatoza
elfu 30 kwa huduma hiyo na hakuna malipo ya kila mwezi au kila mwaka, hii ni
mhimu sana kwa wewe unaeanza biashara kwa kutumia mtandao wa internet.
Ukishajiunga na
CRDB Internet Banking, nakushauri pia fungua akaunti ya dola. Namna ya kufungua
wala sio vigumu na hauhitaji kuwaza juu ya hili. Kama unayo akaunti ya CRDB
basi unachotakiwa ni kuandika barua kwenda CRDB ukiomba kufungua akaunti ya
dola na hautahitaji kiambatanisho kwani viambatanisho vile vile ulivyovitumia
wakati unafungua akaunti ya shilingi vitatumika hivyo hivyo. Ni mhimu sana
kwako wewe unayeanza biashara kutumia internet kufungua akaunti hii ya dola
kwani thamani ya shilingi yetu huporomoka kila wakati. Kwa hiyo kama una dola,
thamani ya shilingi ikiahuka basi wewe ya kwako imepanda.
Kuna rafiki yangu
mmoja aliwahi kuniuliza akaunti ya dola inaonekanaje namba zake? Jibu ni kuwa
siwezi kujua benki zingine namba zinasomekaje ila kwa CRDB ninafahamu. Mfano
kama akaunti yako ya shilingi inasomeka hivi 01j20xxxxxxxx basi akaunti yako ya
dola itasomeka hivi 02j20xxxxxxxx, umeona? Kinachofanyika ni kubadilika namba
moja tu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhali toa mchango au maoni yako hapa