24 May 2015

Jinsi ya kujiunga na mifumo ya PayPal na Moneybookers.


Ndio, kabla hatujaangalia namna ya kujiunga na paypal au moneybookers, hebu na tuangalie pros and cons (faida na hasara) za kutumia kadi yako kwwnye manunuzi mtandaoni, na kwamba paypal au moneybookers ni mkombozi wako.

·         Kwanza tambua kuwa, mtu akizifahamu namba za kadi yako anaweza kuchukua pesa zote kwenye akaunti bila ridhaa yako. Kwa kadi za visa hata mastercard kuna namba namba zimepangwa nne kwenye mafungu manne na zinaunda idadi ya tarakimu 16 (zinaitwa credit card number) na pia zinafuatiwa na namba zingine tatu upande wa nyuma wa kadi (zinaitwa card veeification code). Hizi namba ni mhimu kuzificha kila unapofanya shughuli yoyote kuhusiana na hiyo kadi yako.

·         Pili, utakwepa vipi maana ili ununue ni lazima utaingiza hizo namba zote kwenye mfumo ule unaotumika kununua bidhaa au huduma, utakwepaje sasa? Haupo salama sana kwani endapo muuzaji akiamua kukurudia atakuchukulia pesa maana tayari umeshampa details mhimu za kadi yako.

PayPal

Huu ni mfumo unaomilikiwa na soko la ebay, ni mfumo uliotapakaa karibu kila soko la bidhaa au huduma mtandaoni. Taratibu za kujiunga ni kwenda kwenye tovuti yao www.paypal.com ambapo utajisajili na kupata akaunti. Kawaida yao watakata pesa kiasi cha dola moja na nusu kwa wakati huu naandika wanakata hivyo, kama utasoma maelezo haya wakati ambao imebadilika tafadhali usinihukumu. wanafanya hivyo ili kuhakiki akaunti yako na watairudisha ndani ya siku thelathini. Baada ya kukukata hicho kiwango cha pesa, watakutumia tarakimu nne kwenye statement ya akaunti yako. Ila usije ukasumbuka kwenda benki kuomba statement ukitegemea utauona huo muamala na hizo tarakimu kwenye statement yako, ni kwamba hautauona. Unaweza kuziona tu kwa njia ya internet kwa wale waliojiunga na ebanking.
Baada ua kuukamilisha huo mchakato sasa uko tayari kufanya malipo kwa njia salama kwani paypal hawatahitaji uweke namba za kadi yako kila unapotaka kununua na hawatatoa hizo namba kwa muuzaji.

Moneybookers

Taratibu za kujiunga na moneybookers zinafanan na zile za paypal. Ingia kwenye tovuti yao www.moneybookers.com na ujiunge. Tofauti na paypal ambao hukata kiwangi cha pesa na kukutumia tarakimu nne, monebookers wao huchukua kiwango cha pesa na kukuuliza utaje umekatwa kiasi gani kutoka kwenye akaunti yako. Ki msingi wanataka wahakikia kama kweli akaunti ni ya kwako maana kama sio yako hautajua kiwango gani kimekatwa.

Sasa hapa ndio utaona umuhimu wa kuwa na akaunti ya dola kwani kama unatumia akaunti ya shilingi hautajua ni dola ngapi zimekatwa hata kama utajua dola imeuzwa bei gani siku hiyo. Kwa hiyo ni muhimu kufungua akaunti ya dola na pia kujiunga na internet banking ili kukwemba usumbufu mwingine usio wa lazima. Lakini usiogope unaweza ukaachana na monebookers na ukabaki na paypal sio mbaya. Kwanza paypal ndio inatumika sana kuliko moneybookers.


Hadi hapo naamini tayari umeshangua akaunti paypal na/au monebookers, nakupongeza. Sasa upo salama unapokuwa ukifanya manunuzi yako mtandaoni. Sio kazi ngumu sana japo wengine inawapa shida, ukishindwa basi tupe kazi tukufanyie. Ingia kwenye ukurasawetu wa nyumbani  na ujaze fomu ya oda nasi tutaipata na tutakuhudumia.

Elimu ya manunuzi kwenye mtandao: Anza sasa



Ki msingi sio jambo la kuamka tu siku moja ukaanza kununua kwenye mtandao, ni lazima upitie hatua kadhaa kabla ya kuanza rasmi kununua kwenye mtandao. Jambo la kwanza, fungua akaunti katika benki yoyote yenye huduma za kimataifa kama vile CRDB, NBC, EXIM BANK nk ambazo zina huduma za master card na visa. Kwa NMB hadi niandikavyo maelezo haya ni kwamba hawana huduma za mastercard na/au visa. Ukishafungua akaunti hakikisha unapewa ile kadi ya ATM (credit/debit card), mara nyingi benki zetu Tanzania hutoa debit cards.

Sasa baada ya kuwa umeshafungua akaunti kwenye bank yoyete kisha ukapata kadi ya atm yenye nembo ya mastercard na / au visa, kinachofuata rudi bank uwaombe ili waiwwzeshe akaunti yako kufanya malipo kwwnye mtandao (online purchaising). Bank watakupa fomu maalumu utaijaza kisha ujikomiti kwa lolote litakalotokea katika shughuli yako ya kulipa kwenye mtandao, utaweka sahihi yako kisha wakabidhi hiyo fomu na utaambiwa kusubiri kwa muda usiopungua siku tatu (wakati mwingine unawwza kusubiri hadi mwezi mzima kutegemea na uharaka wa benki husika).

Kuna watu wengi waliwahi kuniuliza ni bank gani inafaa kuitumia kama debit card issuer kwenye manunuzi mtandaoni. Jibu sio rahisi kupatikana maana sijawahi kutumia banki zote, hata hivyo mimi ni mteja wa CRDB na ninazo sababu za kupenda kutumia CRDB. Hebu angalia mfano Standard Chartered au Exim Bank, hutakiwi kufungua akaunti kule kama wewe ni mtanzania mwenye kipato cha chini au kawaida. Huduma zao ni ghali sana na hakuna huduma ya bure. Wakati huu naandika maelezo haya, Standard Chartered wanatoza dola kumi kila mwezi kutoka kwenye akaunti yako pamoja na asilimia zingine zaidi kila unapotumia huduma zao. Kwa CRDB hayo malipo hayapo, hukatwi hela hizo. Mimi sio afisa wa CRDB ila ni mteja na ninaongea na jamii yenye utambuzi na uhuru wa kuchagua huduma toka benki yoyote.

Baada ya kuwezeshwa kadi yako sasa unastahili pongezi maana unaweza kununua unachotaka kutoka mtandaoni na kwa muda wowote hata kama umelala kitandani. Lakini pia sio kulipa tu bali hata kulipwa au kupokea malipo kwa njia hiyo ya kadi yako (Jinsi ya kupokea malipo kwa paypal na moneybookers). Lakini pia lazima ukumbuke kuwa kuna mitandao mingine sio salama kufanya malipo kwa kadi yako, unaweza ukalipa ukajikuta pesa yote haimo kwenye akauntu na utalia. Hivyo imekupasa kuchukua tahadhali kubwa na kuangalia mitandao unayotumia kununua au kulipa. Na ili uwe salama na pesa yako kwa asilimia nyingi, zipo njia na mifumo salama unayopaswa uitumie kwa usalama wa pesa zako.

Ushauri wangu, jiunge na ebanking, mimi ni mteja wa CRDB hivyo sijui benki zingine wanaitaje hiyi huduma. Ukishajiunga na ebanking utaweza kupokea, kutoa au kutumia pesa kwenye akaunti yako kwa njia ya mtandao kwa kutumia komputa au simu yako kama imeunganishwa naaa internet. Hadi naandika maelezo haya ni kwamba CRDB wanatoza elfu 30 kwa huduma hiyo na hakuna malipo ya kila mwezi au kila mwaka, hii ni mhimu sana kwa wewe unaeanza biashara kwa kutumia mtandao wa internet.

Ukishajiunga na CRDB Internet Banking, nakushauri pia fungua akaunti ya dola. Namna ya kufungua wala sio vigumu na hauhitaji kuwaza juu ya hili. Kama unayo akaunti ya CRDB basi unachotakiwa ni kuandika barua kwenda CRDB ukiomba kufungua akaunti ya dola na hautahitaji kiambatanisho kwani viambatanisho vile vile ulivyovitumia wakati unafungua akaunti ya shilingi vitatumika hivyo hivyo. Ni mhimu sana kwako wewe unayeanza biashara kutumia internet kufungua akaunti hii ya dola kwani thamani ya shilingi yetu huporomoka kila wakati. Kwa hiyo kama una dola, thamani ya shilingi ikiahuka basi wewe ya kwako imepanda.

Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniuliza akaunti ya dola inaonekanaje namba zake? Jibu ni kuwa siwezi kujua benki zingine namba zinasomekaje ila kwa CRDB ninafahamu. Mfano kama akaunti yako ya shilingi inasomeka hivi 01j20xxxxxxxx basi akaunti yako ya dola itasomeka hivi 02j20xxxxxxxx, umeona? Kinachofanyika ni kubadilika namba moja tu.


Fahamu maana ya biashara kwa njia ya intaneti (E-Commerce)

Je, umekuwa ukijiuliza nini maana halisi ya kufanya biashara na kupata kipato kupitia intanet? Au pengine ulikuwa ukijiuliza maswali mengi kuwa unaanzaje kuuza au kununua kwenye intaneti? Hapa utajifunza na kufahamu maana halisi ya ecommerce na jinsi inavyofanya kazi. Mwisho wa siku utakuwa muuzaji au mnunuaji kupitia intaneti. Na kwa maana hiyo utakuwa miongoni mwa mamilioni ya watu ambao wamekamata fursa za kibiashara kutumia intaneti.

Maana ya ecommerce ni kitendo cha kuuza au kununua bidhaa na/au huduma kwa njia ya intaneti. Shughuli hii haijaanza leo bali ilianza miaka ya 1960 baada ya kuibuka teknolojia iitwayo Electronic Data Interchange (EDI) ambapo mfumo huo uliwezesha makampuni au watu kuweza kubadilishana hati, hundi au risiti za kibiashara kwa kutumia komputa zilizounganishwa na intaneti. Shughuli hiyo ilishika kasi zaidi kufikia miaka ya 1990 na mwanzo wa 2000. Mfano mwaka 1995, mtandao wa amazon.com ulianzishwa kwa madhumuni ya kuuza vitabu. Mwaka huohuo mtandao wa ebay.com ulianzishwa ukitoa uwezo wa mtu kuuza bidhaa kwa mtu mwingine. Kwa sasa mitandao hiyo imekua sana kulingana na ongezeko la wadau kutoka duniani kote.

 Makundi makuu ya ecommerce 

 B2B (Business to Business)
 Ni mfumo wa biashara unaohusisha wenye viwanda wakiwauzia wafanya biashara wakubwa wanaouza kwa jumla au kiwanda kwa kiwanda wakiuziana au mfanya biashara wa jumla akimuuzia mfanya biashara mwingine auzaye kwa jumla. Mfano wa masoko hayo ya B2B ni kama alibaba.com, made-in-china.com, globalsources.com, tradett.com na mengine mengi.

 C2C (Consumer to Consumer)
 Huu ni mfumo wa kibiashara ya intaneti ambao unahusisha mtu na mtu wakiuziana bidhaa moja au zaidi. Hapa unaweza kuuza au kununua bidhaa ya aina yoyote hata kama ni ndogo na kwa thamani ndogo. Mfano wa masoko haya ni kama aliexpress.com, ebay.com, craiglist.com, etsy.com na mengine mengi.

 B2C (Business to Consumer)
 Kundi hili linahusisha wauzaji wakubwa au viwanda kuwauzia makundi ya wateja aina zote. Hapa pia hutumika mifumo ambayo hakuna mtu katikati wa kuweza kumwuliza (hadi ikibidi) kwani kila kitu unakuta kimewekwa bayana na hiyo mifumo. Mfano amazon.com na masoko mengine.

 C2B (Consumer to Business)
 Hapa unakuta mtu binafsi (consumer) anaweka bidhaa yake kwa njia ya mnada, kisha makampuni yanashindana dau. Baadae huyu muuzaji binafsi anachagua kampuni gani aiuzie hiyo bidhaa. Mfano wake ni kama elance.com na mengine.

Baada ya kuyaona na kuyatambua hayo makundi ya masoko ya kwenye mtandao, sasa hatua inayobaki ni aidha kujisajiri kwenye soko moja au zaidi kama muuzaji au mnunuaji. Kila soko lina namna yake ya kujiunga na pia lina sera tofauti na jingine. Kwa hali hiyo utakapoamua kujiunga utaangalia kanuni na masharti ya soko husika ili uweze kufanya biashara bila shida yoyote. Pia mifano ya masoko niliyoitoa hapo juu haimanishi kuwa hiyo ndio jumla ya masoko yote duniani, hapana, yapo mengi sana. Hata hapa Tanzania kwa mfano kuna masoko kama zoom, kupatana.com ambayo ni C2C marketplaces. Ukishaamua kufanya biashara kwa intaneti utagundua masoko na fursa nyingine nyingi zaidi.